JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/J/112

28 Machi, 2018

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara Zinazojitegemea, Taasisi za Umma mbalimbali Serikalini, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini – RITA, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi wazi za kazi 113 kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.

1.1 AFISA UTAFITI KILIMO DARAJA LA II (AGRICULTURAL RESEARCH OFFICER II) – NAFASI 4 (Agronomy Nafasi 1,

Horticulture Nafasi 1, Agricultural Economics and

Agribusiness Nafasi 1 na Agriculture General Nafasi 1) 1.1.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kusaidia kuandika na kukusanya ripoti za utafiti wa Kilimo/Uchumi kilimo chini ya maelekezo ya afisa utafiti mwandamizi,

ii.

Kukusanya, kurekodi na kuchanganua takwimu za kazi za utafiti zinazoendelea,

iii.

Kuhudhuria mikutano ya Kanda ya kuhuisha programu za utafiti,

iv.

Kusaidia katika kuendesha semina na kuwaelekeza wakulima jinsi ya kutumia teknolojia mpya kwa kuzingatia hali ya uchumi na mazingira yao,

v.

Kutoa ripoti ya maendeleo ya utafiti na mapendekezo ya utafiti katika mikutano ya kanda ya kuhuisha program za utafiti,

vi.

Kufanya shughuli za utafiti chini ya maelekezo na uangalizi wa Afisa mwandamizi,

Utafiti

vii.

Kuandika mapendekezo ya utafiti chini ya uongozi wa Afisa Utafiti Mwandamizi,

viii.

Kuandika ripoti za miradi ya utafiti kwa ajili ya kupitishwa na Afisa utafiti mwandamizi,

ix.

Kufanya majaribio ya husishi ya kilimo ma mifugo katika mashamba ya wakulima kwa kushirikiana na Maafisa Ugani na wakulima wenyewe na

x.

Kufanya kazi zozote kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.

1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (Bachelor Degree) ya Agronomy, Horticulture, Agricultural Economics and Agribusiness na Agriculture General kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali. 1.1.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D. 1.2 DEREVA MITAMBO (PLANT OPERATOR) – NAFASI 1 1.2.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kuendesha mitambo chini ya usimamizi wa Dereva mitambo mwenye uzoefu.

1.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wenye cheti cha kidato cha nne ambao wana leseni Daraja la “G” ya kuendesha Mitambo na ujuzi wa kutunza vyombo mbalimbali vya mitambo hiyo, wenye uzoefu wa kuendesha mitambo kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali. 1.2.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS A. 1.3 FUNDI SANIFU - MAJENGO (TECHNICIAN II ARCHITECTS) – NAFASI 1 1.3.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kufanya kazi kwa vitendo katika fani zinazomhusu ili kumwezesha kupata sifa za kutosha kusajiliwa na Bodi ya Usajili inayowahusu Wasanifu majengo,

ii.

Kufuatilia upatikanaji wa taarifa na taaluma za usanifu wa majengo,

iii.

Kupitia mapendekezo ya miradi (project proposals) mbalimbali ya majengo yanayowasilishwa Wizarani.

1.3.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wenye mojawapo ya sifa zilizotajwa hapa chini: i.

Waliohitimu kidato cha iv na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani ya usanifu majengo

ii.

Waliohitimu kidato cha vi na kufuzu mafunzo ya ufundi wa miaka miwili kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani za usanifu majengo

iii.

Wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Hatua ya I kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali,

iv.

Wenye Stashahada ya kawaida katika fani za ufundi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. 1.3.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C. 1.4 MPISHI DARAJA LA II (COOK GRADE II) – NAFASI 1 1.4.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kusafisha jiko

ii.

Kupika chakula cha kawaida

1.4.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV waliofuzu mafunzo ya cheti yasiyopungua mwaka mmoja katika fani ya ‘Food Production’ yanayotolewa na Vyuo vya Forodhani (Dar es Salaam), Masoka (Moshi), Arusha Hotel, Y.M.C.A (Moshi), VETA (Mikumi) na Vision Hotel (Dar es Salaam) au vyeti vingine vitakavyotambuliwa na Serikali na wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopunguja miaka (3) mitatu.

1.4.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali. 1.5 MJIOLOJIA DARAJA LA II (GEOLOGIST GRADE II) – NAFASI 1 1.5.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kupokea na kufuatilia upatikanaji wa taarifa za utafiti wa mistari ya Uchungi na Mitetemo katika utafutaji wa madini au petrol,

ii.

Kukusanya na kuchambua taarifa za Mitetemo, mienendo na mabadiliko ya miamba ardhini,

iii.

Kutunza kumbukumbu za miamba, madini au petrol,

iv.

Kutayarisha Rasimu za Taarifa za kitaalam na kuziwasilisha kunakohusika,

v.

Kusimamia matumizi ya Vifaa vya Kitaalam na Utunzaji wake, na

vi.

Anaweza kuongoza timu ya mafundi sanifu wanapokuwa katika shughuli za utafutaji wa madini au petrol.

1.5.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wenye Shahada ya Sayansi katika Fani ya Jiolojia (pamoja na fani za Jiofizikia au Jiokemia) au sifa nyingine zinazolingana na hizo kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali. 1.5.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E 1.6 MKUFUNZI DARAJA LA II - KILIMO (AGRICULTURAL TUTOR II) – NAFASI 1 1.6.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kufundisha somo la kilimo katika vyuo vya maendeleo ya wananchi.

ii.

Kutayarisha mpango wa kazi wa Mafunzo

iii.

Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo

iv.

Kutunza vifaa vya kufundishia

v.

Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti

vi.

Kutoa Ushauri wa kitaalam

vii.

Kuandaaa kanuni na taratibu za kusimamia Mitihani chuoni

viii. ix.

Kutunga na kusahihisha Mitihani Kufanya Utafiti utakosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbalimbali katika jamii inayoizunguka chuo

x.

Kutoa Ushauri juu ya kuboresha Taaluma chuoni na kuendeleza Mafunzo nje ya chuo

1.6.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/stashahada ya juu katika somo la kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. 1.6.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D 1.7 AFISA MAMBO YA NJE DARAJA LA II (FOREIGN SERVICE OFFICER II) – NAFASI 2 1.7.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kuandaa Muhtasari, nakala na taarifa zinazohusu masuala ya kimahusiano ya kimataifa.

ii.

Kuhudhuria mikutano mbalimbali.

iii.

Kuandaa mahojiano.

iv.

Kufuatilia masuala mbalimbali ya kimataifa.

v.

Kufanya utafiti juu ya masuala mbalimbali yanayohusu uchumi, siasa na jamii.

vi.

Kutunza kumbukumbu za matukio mbalimbali.

1.7.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa (B.A) ambao wamejiimarisha (major) katika fani ya uhusiano wa Kimataifa (international Relations), Sheria au Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

Aidha wawe

wamefanya na kufaulu mtihani unaotolewa Chuo cha Diplomasia, Dar es Salaam. 1.7.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D 1.8 MTUNZA NYUMBA DARAJA LA III – NAFASI 1

1.8.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kuandaa vitanda,

ii.

Kuhakikisha Usafi wa nguo (linen), Mapazia na mazulia,

iii.

Kusimamia utunzaji wa bustani na ukataji majani (state lodge).

1.8.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiliwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada ya Home Economics au Sifa inayolingana na hiyo kutoka kwenye Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. 1.8.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C. 1.9 DOBI DARAJA LA II – NAFASI 1 1.9.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kufanya uchambuzi wa nguo kwa ajili ya kuosha, kukausha, kunyoosha na kuzifungasha.

1.9.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofuzu mafunzo ya miaka miwili au mitatu katika fani ya Dobi (Laundry Services) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. 1.9.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS. C

1.10

MPIGA CHAPA DARAJA LA II (PRINTER GRADE II) – NAFASI 1

1.10.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kupanga ratiba ya kazi,

ii.

Kuandaa Vifaa vya kufanyia Kazi,

iii.

Kugawa kazi kwa Watumishi walio chini yake,

iv.

Kufuatilia utekelezaji wa kazi zinazoendelea na kutoa taarifa kwa msimamizi wa kazi,

v.

Kutayarisha vielelezo (job jacket lay-out) kuhusu mtiririko wa kazi (Plan of production).

1.10.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wenye Stashahada (Diploma) ya kawaida ya Kupiga Chapa, kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali wenye uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu (3).

1.10.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C

1.11

MPIGA CHAPA MSAIDIZI (ASSISTANT PRINTER) – NAFASI 1

1.11.1 MAJUKUMU YA KAZI Mtumishi katika daraja hili atakuwa katika mafunzo ya kazi chini ya usimamizi wa Wapiga Chapa wenye uzoefu na kupangiwa Kazi zifuatazo; i.

Kukunja karatasi ngumu na kutengeneza ‘covers’ za vitabu, majarida, madaftari katika mahitaji mbali mbali kwa kugandisha, kuweka pamoja au kushona katika hali mbalimbali za ubora,

ii.

Kukarabati vitabu, kumbukumbu mbalimbali au majarida kwa kuyawekea gamba jipya au kurudisha katika hali yake ya mwanzo kutegemea na kifaa hicho kilivyoharibika,

iii.

Kupanga vifaa vilivyotengenezwa katika makasha kwa vipimo vyake au katika seti,

iv.

Kuendesha mashine za kukata karatasi/ kupiga Chapa/ Mashine za Composing, kushona au kugandisha vitabu, majarida, madaftari na vifaa vingine vinavyokuwa vimetakiwa kwa mtindo wa ubora wake,

v.

Kupanga karatasi zitakazochapwa kwa hesabu ya kila kitabu, jarida, daftari na vinginevyo kwa kushonwa au kugandishwa pamoja.

1.11.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au cha Sita waliofaulu masomo ya Sayansi au Sanaa, wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la I (Trade Test Grade I) katika Lithography/ Composing/ Binding/ Machine Minding, au waliohitimu mafunzo ya miaka miwili ya Kupiga Chapa.

1.11.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B

1.12

MHUDUMU WA JIKONI DARAJA LA II (KITCHEN/ MESS ATTENDANT) –

NAFASI 5 1.12.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kusafisha Vyombo vya kupikia.

ii.

Kusafisha Vyombo vya kulia chakula.

iii.

Kusafisha Meza itumiwayo kwa kulia chakula.

iv.

Kuwatayarishia Wapishi/Waandazi vifaa vya Mpishi na Mezani.

v.

Kusafisha maeneo ya kulia chakula na kupikia.

vi.

Kuwasaidia Waandazi na Wapishi.

1.12.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitatu. 1.12.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A 1.13

DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 51

1.13.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,

ii.

Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi,

iii.

Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,

iv.

Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,

v.

Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari,

vi.

Kufanya usafi wa gari na,

vii.

Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

1.13.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha (IV) na leseni ya Daraja E au C1 ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. Waombaji wenye cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza.

1.13.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B.

1.14

MSAIDIZI WA HESABU (ACCOUNTS ASSISTANT) - NAFASI 15

1.14.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za uhasibu;

ii.

Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha;

iii.

Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu;

iv.

Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki; na

v.

Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za Benki na Amana.

1.14.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wenye Cheti cha ATEC level II au “Foundation Level” kinachotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

1.14.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B

1.15

MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III (BASIC TECHNICIAN) – NAFASI

22 1.15.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi

ii.

Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi

iii.

Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha

iv.

Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori

v.

Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali

vi.

Kufanya usafi na ulinzi wa kambi

vii.

Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi

viii.

Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani

ix.

Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na kukusanya takwimu zao

x.

Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya Nchi

xi.

Kudhibiti wanyamapori waharibifu

xii.

Kudhibiti moto kwenye hifadhi

xiii.

Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake

1.15.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Astashahada ya Uhifadhi Wanyamapori (Basic Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. 1.15.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali 1.16

MHANDISI RADIO DARAJA LA II (RADIO ENGINEER II) – NAFASI 1

1.16.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Uendeshaji wa mitambo ya Radio chini ya usimamizi wa wahandisi wazoefu.

ii.

Matengenezo madogo madogo ya mitambo ya Radio.

iii.

Anaweza kuteuliwa kuwa kiongozi wa zamu “Shift Leader”.

iv.

Kuchunguza, kuchambua na kurekebisha mitambo ya Radio

v.

Kusimamia na kuongoza Mafundi Mitambo walio chini yake.

1.16.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wenye Shahada ya Juu ya Uhandisi kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya Uhandisi wa Radio.

1.16.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS. E.

1.17

TABIBU DARAJA LA II (CLINICAL OFFICER II) – NAFASI 1

1.17.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kazi zote zinazofanywa na Tabibu Msaidizi,

ii.

Kutambua na kutibu magonjwa ya kawaida,

iii.

Kusimamia utendaji wa watumishi walio chini yake na kufanya upasuaji mdogo,

iv.

Kutoa Elimu ya Afya kwa jamii,

v.

Kushiriki katika kupanga na kutekeleza Huduma za Afya ya msingi,

vi.

Kushauri na kuhamasisha wananchi kuchangia huduma za afya na mfuko wa afya ya jamii,

vii.

Kuweka kumbukumbu za vifaa na zana za kutolea huduma,

viii.

Kuweka kumbukumbu, kuandaa na kutoa taarifa za utekelezaji,

ix.

Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

1.17.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha nne (IV) au sita (VI) waliofaulu Kozi ya Stashahada ya Utabibu ya miaka miwili (kidato cha sita) au miaka mitatu (kidato cha nne) katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali. 1.17.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia viwango vya mishahara vya vya Serikali . . 2.0 WAKALA WA USAJILI, UFILISI NA UDHAMINI – RITA Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini – RITA ni Wakala wa Serikali ulianzishwa chini ya Sheria ya Bunge Na.30 ya Mwaka 1997 kufuatia Tangazo la Serikali Na. 397 ya tarehe 2/12/2005. RITA Ina jukumu la kuhakikisha ufanisi katika usimamizi wa taarifa ya Matukio Muhimu ya Binadamu na huduma za Ufilisi na Udhamini Tanzania. Wakala unatafuta Watanzania wenye sifa kujaza nafasi zifuatazo; 2.1 AFISA USAJILI MSAIDIZI DARAJA LA II – NAFASI 3

2.1.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kusajili Ndoa, Vizazi na Vifo na Muungano wa Wadhamini na kutunza kumbukumbu zake.

ii.

Kukusanya ada za Ndoa, Vizazi na Vifo na Muungano wa Wadhamini.

iii.

Kutayarisha Fahirisi (Index) za Ndoa, Vizazi na Vifo kwa wilaya na mikoa.

iv.

Kutayarisha matangazo yahusuyo shughuli za mirathi yanayotolewa katika gazeti la Serikali na hati za malipo mbalimbali kuhusu mirathi.

v.

Kutunza magazeti ya Serikali, nyongeza za Sheria (Acts Supplements).

vi.

Kutunza Ratiba za kesi za Mahakamani zinazohusu mirathi (Court Diary) na kuwakumbusha Mawakili wa Serikali wanaohusika.

vii.

Kupokea taarifa na kufanya upekuzi.

viii.

Kuwaelekeza wananchi kuhusu utaratibu wa kuendesha mirathi.

2.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wenye stashahada ya Sheria (Diploma in Law).

2.1.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.C

MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE. i.

Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45

ii.

Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii.

Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iv.

Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

v.

Maombi

yote

yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya

kidato cha nne na kidato cha sita vilivyothibitishwa (Certified Copies) kwa wale

waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.

vi.

-

Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

-

Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

-

Computer Certificate

-

Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

-

Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.

Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

vii.

Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU au NECTA).

viii.

Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

ix.

Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

x.

Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

xi.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 11 Aprili, 2018.

xii.

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA

xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;

http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’) MUHIMU: KUMBUKA KUAMBATISHA BARUA YAKO YA MAOMBI YA KAZI ILIYOSAINIWA PAMOJA NA VYETI VYA ELIMU VILIVYOTHIBISHWA (CERTFIED). BARUA HIYO IELEKEZWE KWA

KATIBU, OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA S.L.P 63100 DAR ES SALAAM.

113 EMPLOYMENT OPPORTUNITIES AT THE UNITED REPUBLIC ...

Page 1 of 14. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. OFISI YA RAIS. SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA. Kumb. Na EA.7/96/01/J/112 28 Machi, 2018. TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI. Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara. Zinazojitegemea, Taasisi ...

361KB Sizes 17 Downloads 326 Views

Recommend Documents

EMPLOYMENT OPPORTUNITIES AT OCCUPATIONAL SAFETY ...
There was a problem previewing this document. Retrying... Download. Connect more apps... Try one of the apps below to open or edit this item. Main menu.

EMPLOYMENT OPPORTUNITIES AT OCCUPATIONAL SAFETY AND ...
vi. Watakaowasilisha taarifa na sifa za kugushi watachukuliwa hatua za. kisheria. Page 3 of 5. EMPLOYMENT OPPORTUNITIES AT OCCUPATIONAL SAFETY AND HEALTH AUTHORITY(OSHA) TANZANIA.pdf. EMPLOYMENT OPPORTUNITIES AT OCCUPATIONAL SAFETY AND HEALTH AUTHORI

74 EMPLOYMENT OPPORTUNITIES AT PUBLIC SERVICE ...
4.1 MAJUKUMU YA KAZI. i. Kufanya kazi za ujenzi wa kuta za nyumba na kupaka rangi na kufunga. mabomba;. Page 3 of 12. 74 EMPLOYMENT OPPORTUNITIES AT PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT.pdf. 74 EMPLOYMENT OPPORTUNITIES AT PUBLIC SERVICE RECRUITMENT

Employment Opportunities-Aquatics.pdf
Sign in. Loading… Whoops! There was a problem loading more pages. Retrying... Whoops! There was a problem previewing this document. Retrying.

Employment Opportunities Oct. 2017.pdf
Princeton University Press. Used. by permission ... 1979 by. Princeton University Press. Used ... Displaying Employment Opportunities Oct. 2017.pdf. Page 1 of 4.

the united republic of tanzania vacancies ... -
and Vocational Training {Tanzania Institute of Education (TIE), Arusha Technical College. (ATC) ...... To develop and implement Division plans and budgets.

New Career Opportunities at Akadeus.pdf
Toulouse Business School - Toulouse. 10 Faculty Positions - ESC Rennes School of Business - Rennes. Program Manager: MSc In Corporate Financial ...

Science and Technology Studies CONSULTANT - Employment at ...
Nov 16, 2014 - Consolidate meeting reports and education material prepared ... held in 2nd and 3rd quarters of 2015, technical meeting on Science and ...

Science and Technology Studies CONSULTANT - Employment at ...
Nov 16, 2014 - Ability to write and edit reports and conference papers pertaining to health and/or education. •. Experience in the development of education ...

113.pdf
Page 1 of 3. 南相馬市. http://www.city.minamisoma.lg.jp/index.cfm/6,17117,26,375,html. 113. . Page 1 of 3. Page 2 of 3. 114. . Page 2 of 3. Page 3 ...

Opportunities at Vidya International Charitable Trust.pdf
Apply online by logging in http://erp.vidyaacademy.ac.in:9191. Applications in hard copy or by e-mail will not be considered. In case of any help needed, please contact Helpline No 9895059911. Page 2 of 2. Opportunities at Vidya International Charita

Challenges And Opportunities In Media Mix ... - Research at Google
Media mix models (MMMs) are statistical models used by advertisers to .... The ads exposure data is more challenging to collect, as ad campaigns are often ... publication can be provided, it is not always a good proxy for the actual ... are well-esti

17_isom_006_Harnessing Inclusive Opportunities Embracing the ...
Page 3 of 3. -3-. (a) PNG and the Digital Age. According to the Business Call to Action - Bridging the digital divide1 PNG the largest. developing economy in the Pacific region, has relatively low penetration rates in the region. Its. challenging ter

Republic of South Africa's Review at the 27th session of the Human ...
May 10, 2017 - made good progress, in particular in the area of socio-economic ... recorded progress in the expansion of its healthcare infrastructure .... It will provide additional tools to investigators and prosecutors to hold the perpetrators of

United States Patent - Research at Google
Sep 30, 2011 - This patent application is a continuation (and claims the. benefit of priority under .... computers, notebook computers, desktop computers, or any.

technical cooperation consultant - Employment at IAEA - Job Application
Planning and organizing skills: Ability to ensure timely delivery of results and to ... analytical content of the Country Programme Framework (CPF) by providing ...

the republic of seychelles in the magistrate court of victoria at ... - SeyLII
Apr 6, 2015 - AT COURT A. VIC-00-CV-CS-0023-2013. (Hearing - Half Day). FABIEN BELLE VS BENJAMIN VERLAQUE. ( C/o : Alexia Amesbury). 09:00 am.

Download [Pdf] Deceived: Star Wars Legends (the Old Republic) (Star Wars: The Old Republic) Read online
Deceived: Star Wars Legends (the Old Republic) (Star Wars: The Old Republic) Download at => https://pdfkulonline13e1.blogspot.com/0345511395 Deceived: Star Wars Legends (the Old Republic) (Star Wars: The Old Republic) pdf download, Deceived: Star

technical cooperation consultant - Employment at IAEA - Job Application
stakeholders, the work of the Department of Technical Cooperation and, more ... analytical, advocacy, communication and operational support for partnership ...

Ray7live! 113.pdf
Songs: The Nicene Creed, We Remember You. Attendance: Samo-chan, Ray, Fusako, Suiko, Sister M, Haru. Introduction to Mark 2. Faith and Reward vs. Sin and Wages. When Jesus saw their faith, he said to the paralyzed man, "Son, your sins are. forgiven."

Republic of the Philippines
pieces passport size picture (colored with white background and complete nametag), 1 piece 1” x 1” picture ... TOTAL NO. PASSED. PERCENTAG. E. PASSED. 1. University of the Philippines - Diliman. 46. 43. 93.00%. 2. University of the East - Manila.